Elimu ya Usuluhishi wa Migogoro ya bima yatolewa visiwani Zanzibar
Elimu ya Usuluhishi wa Migogoro ya bima yatolewa visiwani Zanzibar
Umewahi kujiuliza ukiwa na mgogoro wa Bima unakwenda wapi?
Wananchi mbalimbali wameendelea kutembelea banda la Ofisi ya Msuluhishi wa Migogoro ya Bima (TIO) katika Maonesho ya 12 ya Kitaifa yanayoendelea katika viwanja vya Dimani Unguja, kwa lengo la kupata elimu na ufafanuzi kuhusu huduma zinazotolewa na ofisi hiyo, hususan utatuzi wa migogoro ya bima.
Kupitia maonesho hayo, wananchi wamepata fursa ya kuelimishwa kuhusu majukumu ya TIO, taratibu za kuwasilisha malalamiko ya bima, haki na wajibu wa wateja wa bima pamoja na umuhimu wa kutumia mifumo rasmi ya utatuzi wa migogoro. Maafisa wa TIO wamekuwa wakitoa majibu ya moja kwa moja kwa maswali ya wananchi, hali iliyochangia kuongeza uelewa na imani ya wananchi kuhusu upatikanaji wa haki katika masuala ya bima.
Ushiriki wa TIO katika maonesho hayo ni sehemu ya mkakati wa taasisi wa kusogeza huduma karibu na wananchi, kuongeza uelewa wa umma kuhusu masuala ya bima na kuhimiza wananchi kutumia huduma za usuluhishi pale migogoro inapojitokeza, bila gharama, kwa haki, uwazi na ufanisi.
TIO Suluhisho la Haki la Migogoro ya Bima
