Kamishna wa bima asikiliza mafanikio utoaji elimu TIO ndani ya Maonesho ya Saba Saba
15 Jul, 2025

Julai 13 2025, Kamishna wa Bima Dkt. Baghayo Saqware alisikiliza mafanikio ya Ofisi ya Msuluhishi wa Migogoro ya Bima Tanzania (TIO) katika ushiriki wao wa siku kumi na sita ndani ya Kijiji cha Bima, Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara, Saba Saba na kufurahishwa na ushiriki wao katika utoaji elimu.
Msajili wa Migogoro Bw. Jamal Mwasha alimueleza Kamishna moja ya mafanikio waliyopata ni kuitangaza Ofisi hiyo lakini pia kutoa elimu kwa watanzania ili kujua majukumu ya ofisi hiyo.