Mwenyekiti wa Bodi ya Bima ya Taifa atembelea banda la TIO Maonesho ya Saba Saba
06 Jul, 2025

Mwenyekiti wa Bodi ya Bima ya Taifa CPA Moremi Marwa Julai 4, 2025 alitembelea banda la Ofisi ya Msuluhishi wa Migogoro ya Bima (TIO) ndani ya Kijiji cha Bima na kuelezwa kuhusu utekelezaji wa majukumu mbalimbali ya taasisi hiyo ndani ya kijiji cha bima ikiwemo kutoa elimu ya usajili wa migogoro na usuluhishi wa njia ya haraka na gharama nafuu.