JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

MSULUHISHI WA MIGOGORO YA BIMA

TIRA Logo
Ofisi ya Msuluhishi wa Migogoro ya Bima (TIO) tunashiriki Saba Saba 2025; Karibu Ufahamu majukumu yetu
05 Jul, 2025
Ofisi ya Msuluhishi wa Migogoro ya Bima (TIO) tunashiriki Saba Saba 2025; Karibu Ufahamu majukumu yetu

Maonesho ya Kimataifa ya 49 ya Biashara, Saba Saba yanaendelea jijini Dar es Salaam katika viwanja vya Saba Saba ambapo TIO inashiriki kama jukwaa la kutoa elimu kwa umma kuhusu majukumu yake ambapo leo Julai 04, 2025 wameshiriki katika uzinduzi wa Kijiji cha Bima katika maonesho ya Saba Saba kinachojumuisha watoa huduma mbalimbali za bima.

Aidha, Msuluhishi wa Migogoro ya Bima Bi. Margaret Mngumi katika maonesho hayo akihojiwa na vyombo vya habari alieleza “Bima ni nzuri bima ni salama lakini ikitokea hujaridhika katika kuhudumiwa kwenye bima karibu katika Ofisi ya Msuluhishi wa Migogoro ya Bima ulete changamoto hiyo au mgogoro huo kwa njia ya haraka, rahisi na gharama nafuu”

Ofisi za Msuluhishi wa Migogoro ya Bima Tanzania (TIO) zipo Jengo la Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano 14 – Mtaa wa Jamhuri Gorofa ya chini Dar es Salaam. Wapigie pia kwa namba +255 22 2111117 au watumie barua pepe kupitia msuluhishi@tio.go.tz

#TUNASAJILI NA KUTATUA MIGOGORO YA BIMA KWA NJIA YA HARAKA, RAHISI NA GHARAMA NAFUU