JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

MSULUHISHI WA MIGOGORO YA BIMA

TIRA Logo
Ofisi ya Msuluhishi wa Migogoro ya Bima (TIO) yashiriki Maonesho ya 8 ya Teknolojia ya Madini, elimu yatolewa
28 Sep, 2025
Ofisi ya Msuluhishi wa Migogoro ya Bima (TIO) yashiriki Maonesho ya 8 ya Teknolojia ya Madini, elimu yatolewa

Ofisi ya Msuluhishi wa Migogoro ya Bima (TIO) imeshiriki Maonesho ya 8 ya Teknolojia ya Madini Kitaifa ambayo yanafanyika katika viwanja vya Dkt. Samia Suluhu Hassan, mkoani Geita kuanzia tarehe 18 hadi 28 Septemba 2025.

Kupitia ushiriki huo, TIO imetoa elimu kwa wadau wa sekta ya madini na wananchi kwa ujumla kuhusu majukumu yake, namna ya kufikika, pamoja na aina ya migogoro ya bima inayosuluhishwa. Aidha, wananchi walipata fursa ya kufahamu kwa kina masuala mbalimbali ya bima na mchango wake katika kujilinda na hasara zinazoweza kutokea.

Msuluhishi Mwandamizi kutoka Ofisi hiyo Bw. Aloyce Mbunito alieleza ushiriki wao kwenye maonesho haya ni sehemu ya jitihada za Ofisi hiyo kuendelea kuelimisha jamii juu ya haki na wajibu wao katika mikataba ya bima, sambamba na kuhakikisha migogoro ya bima inatatuliwa kwa haki, uwazi na haraka ili kuongeza imani ya wananchi katika sekta ya bima nchini.

#TIO tunasikiliza na kutatua migogoro ya bima