TIO yakutana na Madaktari wa Hospitali ya Rufaa Amana Kuboresha Ujazaji wa Taarifa za Matibabu
Ofisi ya Msuluhishi wa Migogoro ya Bima (TIO) tarehe 18 Novemba 2025 imekutana na madaktari na wauguzi wa Hospitali ya Rufaa ya Amana kwa lengo la kuitambulisha TIO na kujadiliana kuhusu namna sahihi ya ujazaji wa taarifa za matibabu (Final Medical Reports) kwa upande wa bima.
Aidha akitoa semina hiyo Bw. Aloyce Mbunito Afisa Msuluhishi Mwandamizi kutoka TIO alisisitiza kuwa taarifa hizo ni nyaraka muhimu zinazotumika katika kufanya mahesabu ya kiwango stahiki cha fidia kwa waathiriwa wa ajali wanaopata ulemavu wa muda au wa kudumu.
Pia alisisitiza ni muhimu taarifa hizo zionyeshe kwa usahihi kiwango cha ulemavu (disability percentage) alichopata majeruhi kutokana na ajali, kikilinganishwa na uwezo wake wa kufanya kazi au kipato kabla ya tukio. Asilimia ya ulemavu alizopoteza ndiyo hutumika kama msingi wa kuamua kiwango cha fidia kinacholipwa na kampuni ya bima.
Taarifa za vituo vya afya zikiwa zimeelezwa vyema ni rahisi kwa madai ya bima kulipwa kwa usahihi na hupunguza migogoro ya bima.
#TIO tunasikilza na kusuluhisha migogoro ya bima
