TIO yashiriki mahojiano UTV, yatoa elimu kuhusu utatuzi wa migogoro ya bima

Ofisi ya Msuluhishi wa Migogoro ya Bima Tanzania (TIO) imeshiriki katika kipindi cha mahojiano kilichorushwa na UTV Tanzania Jumatano, Agosti 27, 2025.
Katika mahojiano hayo, Wakili Jamal Hamad Mwasha ambaye ni Msajili wa Malalamiko TIO, alieleza majukumu ya Ofisi hiyo pamoja na faida zake kwa wananchi.
Bw. Mwasha alisema jukumu kuu la TIO ni kusaidia kutatua migogoro ya bima kati ya wateja na kampuni za bima, hasa pale panapotokea kutoridhishwa na huduma au malipo ya fidia.
Aliongeza kuwa TIO pia inatoa ushauri kwa wananchi juu ya njia sahihi za kufuatilia madai yao ya bima. Kuhusu kwa nini mtu mwenye mgogoro wa bima anapaswa kuanza na TIO badala ya Mahakamani, alisema TIO hutatua migogoro kwa haraka, gharama nafuu na kwa mujibu wa sheria ya bima.
Kuhusu njia za kuwasilisha migogoro ya bima kwa walio mbali na ofisi yao iliyopo Dar es Salaam wanaweza wakatuma kwa barua, barua pepe (email) au pia kwenda katika kanda kumi za Ofisi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) na kusajili mgogoro.
Tembelea tovuti yetu ambayo ni www.tira.go.tz na mtandao wa kijamii wa Instagram ambapo wanapatikana kwa jina la tio_tz.
#Tunasajilinakutatuamigogoroyabima