TIO yashiriki Mjadala Kuhusu Ushirikiano, Ubunifu na Usimamizi katika Bima

Ofisi ya Msuluhishi wa Migogoro ya Bima Tanzania (TIO) imeshiriki kwenye Mkutano Mkuu wa Umoja wa Madalali wa Bima (TIBA) uliofanyika leo Septemba 26, 2025 katika Hoteli ya Golden Tulip, Zanzibar.TIO ilishiriki mjadala ulioangazia nafasi ya ushirikiano, ubunifu na usimamizi katika kusukuma mbele maendeleo ya sekta ya bima.
Katika majadiliano hayo, washiriki walipata fursa ya kubadilishana mawazo kuhusu mchango wa TIO katika kulinda maslahi ya wateja wa bima na kushughulikia migogoro inayojitokeza sokoni, ikiwemo changamoto mpya zinazotokana na mabadiliko ya teknolojia na matumizi ya akili bandia (AI).
Msuluhishi wa Migogoro ya Bima, Bi. Margareth Mngumi, alishiriki kama mzungumzaji wa mjadala huo, akisisitiza umuhimu wa mashirikiano baina ya makampuni ya bima, wanunuzi wa huduma, na taasisi za usimamizi ili sekta iwe thabiti na yenye ufanisi.
Mkutano huo wa siku mbili, ulifunguliwa rasmi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi wa Zanzibar, Mhandisi Zena A. Said.
#Tunasikiliza na kutatua migogoro ya bima