TIO yashiriki utoaji elimu kwa mahakimu kuhusu sheria za bima
14 Sep, 2025

Ofisi ya Msuluhishi wa Migogoro ya Bima (TIO) imeshiriki katika semina ya utoaji elimu kwa Mahakimu jijini Dar es Salaam, Septemba 12, 2025, ikiwa na lengo la kuongeza uelewa wao katika kushughulikia madai ya bima.
Katika semina hiyo, Bi. Margaret Mngumi kutoka TIO alitoa elimu kuhusu namna ofisi hiyo inavyotatua migogoro ya bima kwa haraka na kwa gharama nafuu, hatua inayosaidia kupunguza mzigo wa kesi zinazofikishwa mahakamani.
Elimu hiyo inatarajiwa kusaidia Mahakimu kutoa maamuzi sahihi na yenye haki katika mashauri ya bima na hivyo kuimarisha imani ya wananchi katika mfumo wa bima nchini.