JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

MSULUHISHI WA MIGOGORO YA BIMA

TIRA Logo
TIO yatoa elimu ya usuluhishi wa Migogoro ya Bima kwa Wahariri wa Vyombo vya Habari Nchini
25 Nov, 2025
TIO yatoa elimu ya usuluhishi wa Migogoro ya Bima kwa Wahariri wa Vyombo vya Habari Nchini

Ofisi ya Msuluhishi wa Migogoro ya Bima Tanzania (TIO) ilishiriki katika Semina ya bima kwa wahariri iliyoratibwa na TIRA ikiwa na lengo la kutoa elimu ya bima kwa wahariri hao wa vyombo vya habari nchini. Semina hiyo ya siku mbili ilifanyika TIRA - Bima House, Dodoma kuanzia tarehe 18 -19 Nov 2025.

TIO ilishiriki kwa lengo la kutoa elimu ya usuluhuhishi wa migogoro ya bima, sheria na kanuni zinazotumika, migogoro inayopaswa kusajiliwa na masuala mengine mbalimbali. Lakini zaidi wahariri walikaribishwa TIO kufahamu habari mbalimbali ambazi zinaztakiwa kutolewa elimu kwa umma.

Wahariri pia walipata nafasi ya kuuliza maswali mbalimbali kuhusu TIO ambayo yalijibiwa kikamilifu na Msuluhishi wa Migogoro ya Bima Bi. Margaret Mngumi pamoja na Msajili wa Migogoro Bw. Jamal Mwasha