Namna ya kuwasilisha malalamiko
- Malalamiko yawe kwa maandishi (barua au barua pepe) na yaelekezwe kwa Msuluhishi Migogoro ya bima.
- Mlalamikaji aeleze kwa uwazi kiini cha malalamiko yake.
- Nyaraka zote zinazohusu Madai ya Bima na nyaraka za mawasiliano kati ya mlalamikaji na mtoa Bima ziwasilishwe kwa Msuluhishi.
- Mlalamikaji atatakiwa kuwa na subira wakati malalamiko yake yanashughulikiwa na msuluhishi