JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

MSULUHISHI WA MIGOGORO YA BIMA

TIRA Logo
TIO yashiriki Mkutano wa Utoaji Elimu kwa Mawakili wa Serikali Dodoma
11 Oct, 2025
TIO yashiriki Mkutano wa Utoaji Elimu kwa Mawakili wa Serikali Dodoma

Ofisi ya Msuluhishi wa Migogoro ya Bima Tanzania (TIO) imeshiriki katika Mkutano wa Utoaji Elimu kwa Mawakili wa Serikali uliofanyika tarehe 10 Oktoba 2025 katika ukumbi wa Vizano Hotel, jijini Dodoma.

Katika mkutano huo, Msuluhishi wa Migogoro ya Bima, Bi. Margaret Mngumi pia akimuwakilisha Kamishna wa Bima, alitoa wasilisho kuhusu Umuhimu wa ushirikiano wa Mawakili wa Serikali kushirikiana na sekta ya bima katika kutekeleza majukumu yao katika kulinda haki za wananchi.

Aidha, Msajili wa Migogoro TIO Bw. Jamal Mwasha  alieleza kuhusu Sheria mbalimbali pamoja na majukumu ya Ofisi hiyo na upatikanaji wake.

Mafunzo hayo yalifunguliwa rasmi na Mkurugenzi Msaidizi wa Uratibu kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Bw. Ipyana Mlilo, ambaye alisisitiza umuhimu wa mafunzo hayo kwa Mawakili wa Serikali katika kuongeza uelewa wao juu ya masuala ya kisheria yanayohusiana na sekta ya bima na kuhakikisha utoaji wa huduma bora kwa wananchi.

Mkutano huo ulihusisha washiriki kutoka ofisi mbalimbali za kiserikali, ambapo walipata fursa ya kujifunza na kubadilishana uzoefu kuhusu masuala ya sheria, usimamizi na haki za walaji katika sekta ya bima.