Tupo Maonesho ya Nane Nane Dodoma, Karibu ufahamu majukumu ya Msuluhishi wa Migogoro ya Bima
05 Aug, 2025

Ofisi ya Msuluhishi wa Migogoro ya Bima Tanzania (TIO) inashiriki Maonesho ya Kimataifa ya Wakulima Nane Nane yanayofanyika kitaifa jijini Dodoma katika viwanja vya Nzuguni. Maonesho hayo yatadumu kwa siku nane (1 -8, Agosti 2025).
Lengo la ushiriki huu ni kuwaeleza wananchi kuhusu majukumu ya ofisi hiyo ikiwemo kutatua migogoro ya kibima kwa njia ya masikilizano, haraka na kwa gharama nafuu lakini pia jukumu la kusajili migogoro hiyo'
Tupo katika mabanda ya Taasisi za Serikali banda namba 1, Karibu sana tukusikilize.